Tangazo

BURUNDI : Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ubelgiji Didier Reynders aliagiza Wabelgiji wote waishio nchini kurudi makwao, lakini Balozi wa Ubelgiji « anakanusha »

TANGAZO N° 43/2015 LA CHAMA CNDD-FDD LA TAREHE 24 NOVEMBA, 2015

  1. Tarehe 13 Novemba 2015, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ubelgiji, kupitia vyombo vya habari vya RTBF cha Ubelgiji na IWACU ya Burundi aliagiza kwamba Wabelgiji wote waliopo nchini waondoke kwa madai kuwa wanasemwa vibaya na warundi hususan katika tangazo la chama CNDD-FDD na Serikali yake. Baada ya wiki moja ya tangazo hilo, Ubalozi wa Ubelgiji nchini Burundi mnamo tarehe 20 Novemba 2015 baada ya kutafakari kwa kina maagizo hayo walitofautiana na Bosi wao. Balozi alikanusha maelezo hayo na kusema kuwa nchi ya Ubelgiji haijawatolea wito watu wake kuondoka Burundi. Ni dhahiri kuna mitazamo tofauti kati ya mamlaka hizo kuhusu suala hilo, ingawa wote wanatumia njia zisizo rasmi wala sahihi ;
  2. Katika Tangazo hilo la terehe 20 Novemba, 2015,Ubalozi wa Ubelgiji nchini Burundi ulisema kuwa unanzingatia matangazo ya Chama CNDD-FDD na Serikali yake na kwamba wanakumbusha kuwa Ubelgiji ina malengo mahususi na kuafiki mchakato wa mazungumzo kama njia pekee ya kuleta Amani nchini Burundi. Chama CNDD-FDD kinashangazwa na miongozo inayotolewa na Ubelgiji kuhusu mazungumzo ya wananchi kana kwamba ndiyo wenye dira ya mazungumzo hayo. Hali hiyo inaonyesha kwamba hawataki kusikia na kutambua kuwa wao wenyewe ni tatizo la upatikanaji wa amani ya Burundi. Hao ni vikwazo vya demokrasi na maendeleo ya nchi na wananchi wake. Tuamini kuwa adui ndiye atakaye kuwa chanzo cha mazuri ? La hasha!. Kwa maneno mengine mtuhumiwa wa makosa atakuwaje na ukweli kiasi cha kuelekeza dira ya hukumu yake ? Kamwe haiwezekani, kwani chama CNDD-FDD hakikusahau kujulisha katika matangazo yake yote kuwa kwa mtazamo wa Warundi Wabelgiji nao ni kama warundi kwa sababu waliitawala nchi kwa miaka mingi ya ukoloni ;
  3. Mbele ya Ubelgiji yupo Louis Michel na familia yake bila kusahau wanasiasa wa Kikoloni na washirika wake. Hao hawawezi kueleza sababu za Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Didier Reynders mara baada ya kuwataka Wabelgiji kuondoka Burundi, kesho yake magaidi wakarusha mabomu kando ya Radio na Televisheni ya Taifa na kwenye tanki za maji za Regideso, mabomu yaliyogharimu maisha ya watu wasio na hatia. Ubelgiji walikaa kimya kwa sababu waliokufa ni warundi. Kama mauaji hayo yangefanyika katika nchi za Jumuiya ya Ulaya mfano Ubelgiji, mataifa yote yangelaani vikali sana kama inavyofanyika huko Ufaransa. Mtu anaweza kujiuliza kwa nini ukimya huo badala ya kukemea na kulaani ugaidi huo unaopoteza maisha ya Warundi ?. Hii ni dhahiri kwa sababu ni Ubelgiji inayowawezesha kupata pesa na silaha vya kuendeshea ugaidi nchini Burundi ; nao marafiki na washirika wa Ubelgiji wanajikalia kimya. Kana kwamba nchi ya Burundi ilishahukumiwa na kuondolewa kwenye Ramani ya Afrika ;
  4. Matumizi ya maneno ya kuichafua Burundi kuwa kuna mauaji ya kimbari yana asili yake ; kwani magaidi na warushao mabomu dhidi ya wananchi na kuharibu miundombinu tofauti, wanafanya hayo katika ukimya wa Mataifa kana kwamba Burundi haina thamani. Hali hiyo inafanya watu waamini kwamba maneno ya mauaji ya kimbari yaliandaliwa vichwani mwa wanaounga mkono magaidi nchini Burundi. Hayo yanadhihirika katika mikutano ya Kimataifa na matangazo ya mara kwa mara kupitia vyombo vya habari, pale wanasiasa wanaposema kuwa mauaji ya kimbari yanaweza kutokea nchini Burundi, hayo wanayasema wakati ndio wanaounga mkono magaidi na wavunjifu wa amani nchini. Wamepoteza njia na kudhihirisha ubaya wao ! Sasa wametambulika wazi hata kwa aliyekuwa hajui ;
  5. Tangu mwaka 2010, chama CNDD-FDD kinasikitishwa kuona maneno ya mauaji ya kimbari yakisemwa na hao magaidi na washirika wao. Wakati wote wanapotenda uhalifu, wao hutazamia kulipiziwa kisasi ili wadai kuwa ni mauaji ya kimbari yaliyomo vichwani mwao, hivyo iwe ngazi ya kukivunja chama CNDD-FDD na serikali yake. Ni uchokozi wa aina zote wa kuiweka nchi katika matatizo na kutaka kuipindua serikali ambavyo vimekuwa vikitekelezwa bila mafanikio. Lakini mauaji hayo wanayoimba hayatatokea. Pia hadi sasa wanasiasa wakoloni wa Ubelgiji wakiwa pamoja na Louis Michel hawachoki kusema kuwa kuna mauaji ya kimbari nchini Burundi. Hii inaonyesha kuwa maneno mauaji ya kimbari hutumika kama kifaa na silaha vya kuangamiza sawa na silaha nyingine  wazo zitumia kwa malengo ya kukibomoa Chama Cha CNDD-FDD na serikali yake;
  6. Pamoja na maelezo ya maovu yanayotendeka nchini Burundi, mengi yasiyo sahihi, idadi kubwa ya wananchi wa Ubelgiji haiungi mkono siasa hiyo potovu ya Louis Michel, ingawa wanashindwa kuyakanusha hadharani, hali inayojenga hoja ya kufikiria kuwa yamkini wanafanya kazi pamoja naye. Si hayo yaliyosemwa na Ubalozi wa Ubelgiji nchini yenye utata yatakayofanya chama CNDD-FDD kuwa na imani nao. Wala si Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ubelgiji anayetaka kuwalinda magaidi wanaomwaga damu, tukirejea tangazo lake ambalo halikuungwa mkono na Ubalozi wa nchi yake nchini Burundi. Bali chama CNDD-FDD badala yake kinasubiri Ubelgiji kutangaza hadharani kwamba watashiriki mazungumzo ya Warundi, vinginevyo mazungumzo yatakuwa yameegemea upande mmoja kama ilivyokuwa Arusha na penginepo. Mazungumzo kama hayo hayana ufumbuzi wa kudumu.

Tangazo limetolewa Bujumbura, tarehe 24 Novemba, 2015.

na Mheshimiwa Mbunge Pascal NYABENDA,

Mwenyekiti wa Chama CNDD-FDD.

25 novembre 2015

About Author

Willy


Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *