Tangazo

TANGAZO N° 42/2015 LA CHAMA CNDD-FDD LA TAREHE 19 NOVEMBA, 2015

Kutokana na shinikizo la Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel mtoto wa Louis Michel, Didie Reynders Waziri wa Ubelgiji wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ameamuru Wabelgiji waliopo nchini kurudi kwao mara moja.

 

  1. Katika tangazo la chama CNDD-FDD la tarehe 3 Oktoba, 2015, chama kilionyesha kuthamini na masikitiko vilivyosababishwa na kuendelea kutendwa na wakoloni wa Wabelgiji dhidi ya wananchi. Chama kinaomba wananchi wote kuungana kwa pamoja ili waweze kuishtaki nchi ya Ubelgiji katika mahakama za ndani ya nchi na za Kimataifa ili wajibu kwa maovu waliyotenda na wanayoendelea kuwatendea Warundi na Burundi  tangu uhuru wa nchi. Chama CNDD-FDD kiliweka wazi kwamba nchi hiyo inapaswa kujieleza mbele ya wananchi wote kwa matendo yao mabaya. Hayo yafanyike kupitia mazungumzo ya Kitaifa yaliyoandaliwa na Serikali katika ile Kamati ya CNDI na ile ya Ukweli na Maridhiano CVR kabla ya zamu ya Mahakama ;
  1. Chama CNDD-FDD kilisikitishwa kusikia Waziri wa Ubelgiji wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ubeligiji Didiers Reynders kupitia vyombo vya habari vya RTBF na IWACU ya Burundi vya tarehe 13 Novemba 2015, alipowatolea wito Wabelgiji wote kuondoka Burundi bila kukawia kwa visingizio kuwa kuna maneno mabaya dhidi yao huku wakidai kuwa hawapaswi kutajwa kwa matendo   mabaya waliyoifanyia nchi ya Burundi na Warundi tangu Uhuru wao hadi sasa. Hii inabainisha kwamba Waziri huyo aliyafanya kwa shinikizo la Waziri bosi wake ambaye ni mtoto wa Louis Michel, ni dhahiri kwamba wale wanasiasa wa kikoloni Wabelgiji wanafanya watakavyo katika masuala ya Burundi. Ingawa ni hivyo, chama CNDD-FDD kinafahamisha kwamba kazi ya mazungumzo ya Warundi kote nchini na walio nje ya nchi imeshaanza pia Wabelgiji wanahusuka kama Warundi, wanapaswa kushiriki mazungumzo hayo kwani walitutawala miaka mingi ;
  1. Chama CNDD-FDD kinaona kwamba amri hiyo ya kuwarudisha makwao raia wa Ubelgiji kwa nguvu ni njia isiyofaa ili iwaepushe mazungumzo ambayo yameanzishwa, hivyo yale mabaya waliyotendea Warundi na Burundi yasiwekwe hadharani, kwani kwa vyovyote vile wanapaswa kuomba msamaha na kulipa fidia kwa nchi. Kwa mantiki hiyo chama CNDD-FDD kinaona kwamba misaada ya Ubelgiji kwa nchi ya Burundi ilikuwa na walakini/mashaka , badala yake Burundi inastahili fidia muhimu ;
  1. Chama CNDD-FDD kinahuzunishwa na matendo ya wakoloni Wabelgiji na wanasiasa wao wanaounga mkono mawazo hayo ya aibu. Hali hiyo inasikitisha warundi hasa wanapopandikiziwa chuki ya ubaguzi nchini hadi kusababisha mauaji ya halaiki huku wakiangalia tu na kusema kuwa wananchi wanamalizana, hivyo wawekewe vikwazo na kupelekewa askari wa kimataifa, kwa malengo ya kuendelea kuitawala Burundi baada ya vurugu wanazosababisha wenyewe. Mbali na hayo, Chama CNDD-FDD kilisikitishwa na bado kinasikishwa na viboko walivyopigwa wana wa Burundi ambapo wanaume walipigwa mbele ya wake zao, watoto na wakamwana wao ili kupoteza heshima na haki ya Warundi. Hayo si ya kuvumilia, wanapaswa kuyajibu, wasikwepe, kujitenga wala kuyakimbia ;
  1. Mbinu za kukimbia na kutaka kujitoa kabla ya hatua za mkono wa sheria, zinatafsiri maana ya kuunda kundi la kigaidi linalotia hofu katika baadhi ya Kata za Jiji la Bujumbura. Kundi hilo linapewa pesa na silaha ili kuiondoa serikali iliyoko madarakani, lakini limeshindwa. Njia zote hizo ni kutaka kuifanya Burundi idumu katika uvunjifu wa amani na uhasama , ili utawala ukiangushwa iwe sababu ya wale Wabelgiji kusahauliwa, wasifuatiliwe kwa maovu waliyowatendea wananchi. Katika mipango yao mibovu ya kukandamiza uhuru na kujitawala kwa Burundi na kuendesha mambo ya nchi kwa kujiwekea uongozi uliochaguliwa na wananchi, vilitumika pia vyombo vya habari vya nchini na Kimataifa wakati wote wakiunga mkono lile kundi lililokuwa limekusudia kufanya mapinduzi ya tarehe 13 Mei, 2015, jaribio ambalo halikufanikiwa. Hivi sasa hao Wabelgiji na Washirika wao ndio wanaomba kuwa hao waandishi wa habari waachiwe kuendeleza uovu wao wakati ndio waliojiharibia wenyewe na kuamua kuharibu vituo vyao vya redio baada ya kushindwa katika jaribio la mapinduzi hatimaye kukimbilia nchi ya Rwanda ;
  1. Chama CNDD-FDD hakielewi kwa nini mashirika ya habari ya kimataifa wanaendelea kudai kuletwa wasimamizi wa kimataifa wa UN bila kuishirikisha nchi ya Burundi. Ifahamike kuwa Azimio No 2248 (2015) ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Umoja wa Mataifa ilitambua na kuheshimu uhuru na kujitawala kwa Warundi, kuheshimu mipaka ya nchi na Umoja wa Warundi. Hao wanasiasa wengine wanaoendelea kuzingatia fikra za wakoloni Wabelgiji na kuhimiza waandishi wa habari kwenda kinyume na Azimio la Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Umoja wa Mataifa UN ndiyo wamegeuka watawala wa dunia ? ;
  1. Chama CNDD-FDD kinaomba hao wanasiasa wasaliti wa Burundi wakubali makosa kwani njia za kujitakasa ni katika ile Kamati ya Ukweli na Maridhiano CVR na katika ile Kamati ya Mazungumzo ya Kitaifa CNDI. Ingawa Ubelgiji na washirika wake wamesitisha misaada, Chama CNDD-FDD kinajulisha kuwa wananchi ni wazuri na kwamba watawasikiliza, wakijirudi na kuomba msamaha watawaelewa vizuri na hasa wakikubali kusema ukweli na kuudhihirisha. Burundi na Ubelgiji wataanzia hapo kuishi kwa maelewano, kuheshimiana na kuheshimu haki na uhuru wa nchi zote hizo. La sivyo Wabelgiji hawatapata amani mioyoni ikizingatiwa kwamba historia haifutiki ;
  1. Mbali na historia hiyo isiyosahaulika, chama CNDD-FDD kinasikitishwa kuona Ubelgiji ikiongeza ubaya juu ya mwingine kila kukicha kwa kusisitiza Mataifa ya Jumuiya ya Ulaya , Umoja wa Afrika , Umoja wa Mataifa na kutuchonganisha na nchi jirani ambayo ni rafiki . Ubelgiji imekuwa ikifanya hivyo eti ni kwa sababu walitutawala na kutumia mbinu zote ili uongozi uliochaguliwa na wananchi usitishwe na hatimaye kuusambaratisha utawala wa chama CNDD-FDD. Vitisho vya vikwazo vya kiuchumi na uhusiano wa Kimataifa kupitia vyombo vya habari na kuomba Burundi itawaliwe na Jeshi la Kimataifa la UN haviachwi nyuma  na hao Wabelgiji ;
  1. Chama CNDD-FDD kinafuatilia kwa karibu masuala kadhaa na kuona kuwa nchi ya Ufaransa wakoloni wa Senegal, Ivory Coast, Burkina Fasso na nyinginezo ni wakili mzuri wa makoloni hayo katika mataifa mengine, nchi hizo zinapopatwa na matatizo. Kitu cha ajabu ni kuona Ubelgiji daima ikijishughulisha na kutaka kuipindua Serikali ya nchi waliyoitawala, mfano ni Burundi tangu uhuru wake hadi hivi sasa. Tena wakati wote walipounda makundi ya uhalifu walikuwa na malengo ya kutatiza uhuru na kujitawala kwa wananchi. Hayo yalitokea alipouawa Mhanga wa Uhuru Mfalme Louis Rwagasore 1961, wakati Waziri Mkuu Petro Ngendandumwe alipouawa 1965, pia yalitokea wakati Mfalme Ntare V Ndizeye Karoli alipouawa mwaka 1972, hadi leo haijulikani alipozikwa, huyo alifuatiwa na mauaji ya wananchi maelfu na maelfu waliouawa huku Wabelgiji wakiangalia tu ; kwani nao walihusika na maandalizi hayo. Hatuwezi kusahau Mhanga wa Demokrasi Rais Ndadaye Melchior na wasaidizi wake waliouawa mwaka 1993, wakati wote huo uhusika wa Ubelgiji ulionekana. Yaliyotokea tangu 2010 hadi 2015 kuhusiana na zoezi la kutaka kudhoofisha uongozi wa chama CNDD-FDD yamekuwa yakiandaliwa na Ubelgiji na kutekelezwa na kundi wanalounga mkono kama ilivyokuwa inafanyika tangu awali;
  • Kwa kurejea yote tuliyoeleza, chama CNDD-FDD kinaomba wananchi kuendelea kushikamana katika Umoja kwani ndiyo ngao ya kukinga mabaya yote yanayosababishwa na chuki za kikoloni ambazo hazijatoka miongoni mwa baadhi ya wanasiasa wa Ubelgiji. Hii ina maana kwamba mapambano ya kujitawala bado yanaendelea, wananchi waendelee kuwa macho wakizingatia kuwa yale mazungumzo ya wananchi yameanza sambamba na kazi za Kamati ya Ukweli na Maridhiano CVR. Mazungumzo hayo yasiwe kama yaliyofanyika katika nchi nyingine ambapo Wabelgiji hawakushiriki, mfano ni makubaliano ya Arusha ya mwaka 2000, katika mazungumzo ya kusimamisha vita ya 2003 na ndiyo sababu miafaka iliyofikiwa haikudumu. Huu ni wakati wa ukweli kudhihirika, mazungumzo yaanzie kwenye vyanzo vya matatizo ili Nchi ipate uhuru kamili, kujitawala kikamilifu, kuheshimiwa mipaka yake pamoja na Umoja wa Warundi usiokuwa na udanganyifu;

 

 

Tangazo limetolewa Bujumbura, tarehe 19 Novemba, 2015.

 na Mheshimiwa Mbunge Pascal NYABENDA,

Mwenyekiti wa Chama CNDD-FDD.

20 novembre 2015

About Author

Willy


Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *