Tangazo

Chama CNDD-FDD kinashukuru hatua iliochukuliwa na Kamati ya Usalama ya Umoja wa Mataifa (CSNU)

TANGAZO No 40 /2015 LA CHAMA CNDD-FDD LA TAREHE 13 NOVEMBA 2015

  1. Tarehe 12 Novemba 2015, Kamati ya Usalama ya Dunia ilikutana na kuafikiana kwa hatua muhimu N0. 2248 (2015) ya kuisaidia Burundi kumaliza matatizo ya kisiasa na usalama baada ya mikutano mingi na malumbano ambavyo havikuleta mafanikio. Warundi walisubiri kwa shauku kubwa majibu ya suluhu kutoka katika mkutano huo, wanashukuru kwa hatua zilizochukuliwa hususan Chama CNDD-FDD na serikali yake ;

 

  1. Chama CNDD-FDD kinashukuru pia kuwa mataifa yenye nguvu yanayowakilishwa katika Kamati hiyo ya Amani ya UN pamoja na mataifa mengine duniani wamebaini ukweli na kuchukuwa hatua zifaazo kwa matatizo ambayo yamekuwa yakiisibu Burundi. Ni hatua nzuri iliopigwa na mataifa ya kujua ukweli na njia ya ufumbuzi wake maridhawa ;

 

  1. Kama baadhi ya wawakilishi wa nchi zao hapa Burundi wangechunguza kwa makini masuala ya Burundi, migogoro isingefikia hapa. Ni dhahiri baadhi ya nchi zilipewa taarifa zisizo sahihi na wawakilishi wao ; hivyo nchi hizo kuelewa tofauti hali halisi na kuchukuwa hatua zilizo kinyume. Tunaomba nchi hizo kufuatilia kwa makini wasidanganywe tena ;

 

  1. Chama CNDD-FDD kinashukuru kuona kuwa katika hatua zilizochukuliwa, Uhuru wa Nchi na Umoja wa Warundi vimetambuliwa na kuheshimiwa. Haki hiyo ilikuwa imekanyagwa na kuwafanya warundi wasijiongoze na kuweka sawa mambo yao. Chama CNDD-FDD kinaomba kwa msisitizo kuishi kwa uhuru na wananchi kujiamlia masuala yao wenyewe na uwezo wanao . Kwa ujumla hakuna matatizo ya kuwatenganisha warundi ;

 

  1. Chama CNDD-FDD kinatambua na kinashukuru kwa dhati mataifa rafiki walioelewa na kuisema vizuri nchi ya Burundi, wakati baadhi ya nchi walichochea ubaya. Wanachama (abagumyabanga) kamwe hawatavumilia kuingiliwa ;

 

  1. Chama CNDD-FDD kama ulivyo utamaduni wake wa mazungumzo tangu kikiwa Vuguvugu la Ukombozi katika kupata uvumbuzi wa migogoro, kinakubali na kuwaahidi wananchi na mataifa kuwa wako tayari kwa mazungumzo. Chama CNDD-FDD kinaishukuru Serikali yake kwa kipaumbele cha njia ya mazungumzo na kuteuwa Kamati ya Taifa (CNDI) yenye majukumu ya kuandaa na kuendesha mazungumzo kati ya warundi walio nchini hata walio nje ya nchi, na kwamba Serikali haitamtenga yeyote mwenye haki ya kushiriki. Warundi wote nchini na walio nje pamoja na yeyote anayehusika na yaliyoisibu nchi wanaalikwa katika mazungumzo hayo ;

 

  1. Chama CNDD-FDD kimefurahi na kuridhishwa na maamuzi No. 2248 (2015) yaliochukuliwa wakati zoezi la kusaka na kupokonya silaha zinazomilikiwa kinyume na sheria kama ilivyoshauriwa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika katika mikutano mbalimbali likienda vizuri kwa amani, bila usumbufu kwa wananchi. Inadhihirisha kauli ya Mheshimiwa Mkuu wa Nchi alivyotangaza tangu awali kuwa hayatatokea tena mauaji ya kimbali nchini Burundi wakati wowote Chama CNDD-FDD kitakapokuwa madarakani ;

 

  1. Chama CNDD-FDD kinamalizia tangazo hili kwa kuwaomba wananchi wote kusikia vizuri na kuiunga mkono hatua iliochukuliwa, ili kila mwenye hoja aiwakilishe katika mazungumzo hayo yatakayofanyika kwa amani na utulivu kwa kuheshimiana. Chama CNDD-FDD kinatumia fursa hii kumuomba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban – Ki- Moon kusisitiza mataifa yaliositisha missada kwa ajili ya Burundi waruhusu misaada hiyo, kwani watu hawawezi kufanikiwa katika mazungumzo kukiwa na vikwazo vya kusababisha njaa kwa wananchi.

 

 Tangazo limetolewa Bujumbura, tarehe 13 Novemba, 2015

Mbunge Pascal Nyabenda

Mwenyekiti wa Chama CNDD-FDD

13 novembre 2015

About Author

Willy


Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *