Tangazo

Chama CNDD-FDD kinalaani wauaji wenye staili kama Boko Haram, Al-Shebab na Al Qaeda

TANGAZO N° 037/2015 LA CHAMA CNDD-FDD LA TAREHE 14 OKTOBA, 2015

 

  1. Kumekuwa na wauaji wanaotumia risasi na kuwarushia askari polisi mabomu ya mkono pamoja na kuwaua baadhi ya watu, wakati mwingine wauaji hao hutumia pikipiki. Hao wakiungwa mkono na baadhi ya mataifa wahisani, wanawahi kutoa taarifa wakisema kuwa ni masuala ya ukabila. Mfano tarehe 8 oktoba, 2015 aliuawa Pascal Nshimirimana nyumbani kwake Ngagara  ambaye ni mkwe wa Petro Claveri Mbonimpa, watu wa familia yake wakaomba kuwa uchunguzi dhidi ya kifo hicho usifanyike kwa madai kuwa ni matatizo ya kifamilia; mashirika ya habari ya kimataifa na redio wakatoa taarifa kuwa ni sababu za mzozo wa wafanyabiashara. Jumanne mchana  tarehe 13 Oktoba, 2015 katika mtaa wa tatu Kata ya Ngagara Jijini Bujumbura askari watatu (3) walitekwa. Mmoja kati ya mateka aliponyoka na kufikisha habari kwa wenziwe ili wakatoe msaada wa kuokoa waliokuwa mikononi mwa wahalifu. Askari wa usalama walikuta mmoja ameuwawa na mwingine kajeruhiwa sana ;
  1. Katika harakati za kuwakomboa polisi waliotekwa , familia ya mpiga picha wa Televisheni ya Taifa Nkezabahizi Christophe iliokuwa imechukuliwa kama ngao na magaidi hao iliteketea yote kwa lisasi zilizokua zikirushwa. Waliokufa ni mwandishi wa habari huyo, mkewe na watoto wake wawili (2) wenye umri wa miaka 14 na 16. Kwa ujumla, watu 10 wakiwemo magaidi na askari polisi aliyeuliwa na magaidi hao wamepoteza maisha. Chama CNDD-FDD kinatoa salamu za lambilambi kwa familia zote zilizo poteza watu wao. Ila kitu cha kusikitisha ni kwamba baadhi ya Mashirika ya Habari ya kimataifa na redio walieneza taarifa za uongo walizopewa na washirika wao waliopo nchini Burundi kwamba askari wa usalama walishambulia familia ya mwandishi huyo wa habari, huku wengine wakisema kuwa ni suala la ukabila bila uthibitisho wowote ;
  1. Wanaochukulia hoja ya kisiasa ya Burundi wanavyotaka, wanapenda kujinufaisha kwa kutumia ukabila kama njia ya kutatua matatizo ya Burundi. Ikumbukwe kwamba katika mazungumzo ya Arusha ilibainika wazi kuwa migogoro ya Burundi ni ya kisiasa yenye sura ya ukabila. Chama CNDD-FDD katika mazungumzo yake na serikali ya kukomesha vita yaliohitimishwa na makubaliano ya tarehe 16 Novemba, 2003 ilidhihirika kuwa matatizo ya Burundi yalikuwa ya kisiasa. Utashangaa kuona baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa wakitoa taarifa za uongo kuwa matatizo ya Burundi ni ya kikabila, hii inamaanisha kwamba wauaji hao wanaojitioa mhanga kwa kuuwa ndugu zao warundi hususan askari polisi kwa misingi ya kikabila, hayo ndiyo yanayofanywa pia na baadhi ya mataifa  kwa kuunga mkono wauaji hao. Sasa wanadhihirisha azma yao ya mpango wa ubaguzi wa kikabila nchini Burundi ;
  1. Warundi wapenzi wa demokrasi si wajinga pia hawawezi kuficha huzuni yao, kuona wakati wanaadhimisha kumbukumbu ya  miaka 54 ya kifo cha mhanga wa uhuru Louis Rwagasore aliyeuawa  na wenye ubaguzi wa kikabila kama wanavyodai wenyewe ndiyo hao wanaoendeleza mauaji ya askari polisi wa usalama wa nchi. Wakati Mheshimiwa Rais wa Jamhuri  aliagiza kuwa amani iwe imerejea kote nchini katika kipindi cha miezi miwili, ni dhahiri kwamba maadui hao wa nchi wakiungwa mkono na baadhi ya nchi wakiloni hawafurahii umoja na mshikamano wa wananchi na harakati za maendeleo yao, hii ina maana kwamba nchi hizo zinatamani kurudi kuitawala Burundi kupitia ukoloni mamboleo ;
  1. Wakati huu chama CNDD-FDD na serikali yake walikwishatambua kuwa mataifa hayo hayapendi kufanyika kwa mazungumzo kati ya warundi ndiyo maana wanawaunga mkono kwa hali na mali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia silaha wauaji hao ambao inafahamika wazi hawana uwezo wa kuzipata. Ingawa chama CNDD-FDD na serikali daima wanasisitiza kufanyika kwa mazungumzo, mataifa hayo hawataki kufanyika kwa mazungumzo hayo.  Chama CNDD-FDD kinaona kusitishwa kwa msaada ni kutatiza mipango ya Burundi na misaada hiyo ambayo imekuwa ikitolewa, 80% hurudi kwao wakati huo huo Burundi ikitakiwa kuilipa, ni kama kupokea  msaada  ambao robo tatu yake  inarudi  kwao. Wakati huo hatuko katika malumbano ya misaada hiyo kwani  Mungu aliyeiumba nchi ya Burundi anaiona. Shida na matatizo tunayopata ni sababu za hao wanafiki wanaoendelea kuunga mkono magaidi hao kwa lengo la kuisambaratisha nchi. Warundi wamevumilia  muda mrefu, wamevumilia maovu wanayotendewa huku wanaounga mkono wahalifu wakikaa kimya wakijikuna videvu  wakidhani kwamba wataendelea kuwachonganisha warundi  na  kuwa wao hawawezi kuguswa ; ni wakati wa kuwafikisha katika mahakama ya kimataifa.
  1. Chama CNDD-FDD kinamalizia kwa kuomba wanasheria wote wa Burundi kwa kuungana na wananchi, wasimame kwa pamoja  kuunga mkono nchi kwa kushitaki mataifa ya wakoloni  wanaoendelea  kuikandamizia Burundi katika mgogoro na mauaji kati ya warundi  kwa kuunga mkono hao wanaoendelea kusababisha  uvunjifu wa amani nchini, kwani haina mantiki kuona chama CNDD-FDD na serikali yake  wakitekeleza mikakati ya ujenzi wa Taifa huku wengine wakiiharibu. Kuna siku ukweli utadhihirika sheria ichukue mkondo wake dhidi ya  mataifa hayo  hatimaye warundi wawe katika mshikamano wapate amani na utulivu ambavyo ni nguzo ya maendeleo.

  Tangazo limetolewa Bujumbura, tarehe 14 Oktoba, 2015.
  na  Mheshimiwa Mbunge Pascal NYABENDA,

Mwenyekiti wa Chama CNDD-FDD. 

15 octobre 2015

About Author

Willy


Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *