Actualité, Tangazo

TANGAZO No 06 /2016 LA CHAMA CNDD-FDD LA TAREHE 26 Machi, 2016.

Chama CNDD-FDD hakitaketi na wauaji katika Mazungumzo kwa kuheshimu Azimio la UN, No 2248 la tarehe 12 Novemba 2015.

1. Chama CNDD-FDD kiligunduwa kuwa Jumuiya ya Kimataifa inashinikiza kuzungumza na wahalifu walioshiriki katika vurugu na kutaka kuangusha uongozi uliochaguliwa na wananchi. Chama kinaheshimu na kuzingatia Azimio No 2248 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la tarehe 12 Novemba, 2015 linalofafanua wenye haki ya kushiriki mazungumzo, kuwa ni wale ambao hawajashiriki ghasia za kuvuruga amani ya nchi. Yanayotokea kupitia mitandao ya Kitaifa na Kimataifa yanaonyesha wazi kuwa wanaochochea ugaidi hawajasalimu amri na kwamba mamlaka tawala haikufanya kosa kuwaweka wazi ;
2. Tangu hatua za mwanzo za mgogoro hadi kilele cha jaribio la mapinduzi ya tarehe 13 Mei, 2015 pamoja na mwenedelezo wa uvamizi wa tarehe 11 Desemba, 2015, chama CNDD-FDD kilikuwa kikijulisha wananchi na Jumuiya ya Kimataifa ukweli, kwamba maandamano ya ghasia hayakuhusiana na awamu ya urais. Ikumbukwe kuwa siku chache baada ya ushindi wa chama CNDD-FDD 2015, vuguvugu la wapinzani walikimbilia Rwanda na kupewa mafunzo ya kijeshi kwa azma ya kurudi kuvuruga taasisi na kupindua serikali iliochaguliwa na wananchi. Wakati ule hoja haikuwa awamu ya Rais. Mwaka 2010 miongoni mwa wanasiasa wale wale walisusia uchaguzi ili mchakato wake usifanikiwe. Daima suala halikuwa awamu ya uongozi, bali mwendelezo wa usumbufu kwa maandalizi yao ya mauaji ya halaiki. Hata matukio ya 2015 vipindi vya urais haikuwa sababu bali nia ya kutekeleza mpango wa mauaji ulioshindwa 2010. Habari zilisikika kupitia vituo vya redio na mitandao ya kijamii kwa kaulimbiu ya « sasa hivi iwe isiwe Burundi tutaikamata » Yaliyokuwa yamefichwa yako hadharani. Wabunifu, waandaji, watendaji na vitendeakazi na vinginevyo sasa vimebainika. Hapa chama CNDD-FDD kamwe hakikujidanganya wala kuwadanganya wanachama na wapenzi kuwa kulikuwa na njama za Kimataifa dhidi ya Burundi ;
3. Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Kitaifa na Kimataifa yalidokeza kuwepo kwa maandalizi ya makundi kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi. Jumuiya ya Kimataifa ilisimama kinyume ili kulinda maandalizi hayo kwa hila. Waliunda mikakati ya kudunisha chama CNDD-FDD na serikali yake ikiwa ni pamoja na kuandaa mauaji ya halaiki dhidi ya wanachama na chuki miongoni mwa washirika. Ilitajwa mara nyingi kuwa maabara ya mauaji yako nchini Rwanda kwa Paul Kagame aliyezoea kuyafanya nchini mwake. Baada ya majaribio kwake, Kagame anatamani kuhamishia uovu huo na ubeberu nchini Burundi. Hata baadhi ya wanasiasa kama Louis Michel walikuwa wakimwezesha Paul Kagame kwa silaha na pesa wakati rais huyo akifadhili makundi ya warundi ya uasi makambini kwa hifadhi, mafunzo ya kijeshi na mahitaji mengine ; ili waasi hao wapenyezwe kufanya mauaji nchini Burundi kama ilivyokuwa nchini mwake. Wakati waasi walipofanya operesheni katika baadhi ya Kata za Jiji la Bujumbura kama vile Cibitoke, Mutakura, Ngagara, Nyakabiga, Jabe na Musaga walichimbisha mashimo kabla kwa kusubiri mauaji ya halaiki ambayo wangetekeleza kama wangefanikiwa ; ni sawa na mbinu alizotumia Kagame wakati wake alipoamrisha wafuasi wake kuchimba mashimo kusubiri filimbi ya kuanza zoezi aliposhambulia Kigali. Ilishangaza watu kuona mashimo yaliyokuwa yamechimbwa katika familia za wafuasi na wanachama wa Inkotanyi. Shimo lenye kina cha zaidi ya mita 10 kwa ajili ya kutupiwa watakao uawa lilionekana. Ni hivyo, si kwamba nchini Rwanda mashimo yaliandaliwa siku Kagame alipotungua ndege ya Rais Ntaryamira Cyprien! La hasha. Mashimo hayo yalikuwa yameandaliwa mapema, kwani yasingechimbwa kwa siku moja au mbili ;
4. Kazi za baadhi ya wanahabari na mashirika ya habari ya Kimataifa nchini Burundi ilikuwa ni kujifurahisha na kutaka kushuhudia kupinduliwa kwa serikali ya chama CNDD-FDD iwapo ingetokea. Vyombo hivyo havikuzingatia maadili na wajibu wa kazi, hasa kwa uongo uliotumika, kuegamia vuguvugu la waasi na kuhamasisha fujo. Wapenzi wa demokrasi wanaomba vyombo vya habari husika kuwajibika kuhusu hoja za mashimo walimozikwa watu wengi yaliyoanza kuonekana katika Kata za Mutakura na Cibitoke, kwani walikuwa mashuhuda. Waandishi hao mara nyingi walikishutumu chama CNDD-FDD, umoja wa vijana Imbonerakure pamoja na mamlaka za ulinzi na usalama kufanya mauaji ya raia. Hivi sasa mashimo walimozikwa watu yamefichuliwa na kwamba wauaji wa watawa wa Kamenge wamejulikana ikiwa ni pamoja na waliounguza duka kubwa la wachina T2000 kukiri wenyewe uovu huo. Vile vile ubakaji uliosingiziwa vyombo vya usalama imebainika kuwa si kweli, bali ni elementi za waasi kwa mujibu wa waliojisalimisha. Chama CNDD-FDD kinasubiri kuona waandishi hao wakifikishwa mbele ya mahakama za Taifa au za Kimataifa kwa lengo la kukomesha hali ya kutoadhibu makosa ;
5. Baadhi ya asasi za kiraia na vyama vya kisiasa vya upinzani wa demokrasi wanashutumu matangazo ya baadhi ya viongozi wa makanisa Katoriki nchini Burundi. Ni matangazo yenye ujumbe wa hatari kwa mamlaka na taasisi za uongozi uliochaguliwa na wananchi. Kama ilivyo katika tangazo la Hamza Venant Burikukiye kiongozi wa CAPES+, uhusika wa dini Katoriki umekuwa ukijitokeza katika vurugu nchini tangu ujio wa mapadri wa kizungu walioandaa njia ya wakoloni wa Ulaya. Katika tangazo lake Hamza Burikukiye anaonyesha ubia wa Kanisa na utawala wakati wa kifo cha Mfalme Louis Rwagasore, anaonyesha pia nafasi ya Kanisa Katoriki katika mapinduzi ya serikali yaliyotokea nchini hadi sasa, kama ambavyo kipindi cha 1972-1973 pekee Mapadri wengi akiwemo Michel Kayoya waliuawa, viongozi wa dini Katoriki wakichochea na kushangilia. Chama CNDD-FDD hakiko mbali na hayo yaliyotangazwa na CAPES+, kwani baadhi ya washirika wa dini Katoriki ni watuhumiwa wa maafa yaliyoisibu nchi. Mwenendo wa Kanisa Katoriki tangu 2010 hususan kuanzia tarehe 26 Aprili, 2015 unadhihirisha historia ya baadhi ya waumini wa dini hiyo ikiwemo hali isiyopendeza ya baadhi ya viongozi wa dini. Hao walijipa kazi ya kuisumbua Tume huru ya Uchaguzi CENI na kutatiza majukumu ya Kamati ya Ukweli na Maridhiano ya warundi CVR ; yote hayo yalisindikizwa na matangazo ya kuchoma mioyo kupitia ibada makanasani, hivyo kufanya baadhi ya watu kufikiri kwamba Kanisa Katoriki litapoteza mwelekeo badala ya kujenga mioyo na roho za waumini na wananchi kwa ujumla na kuwa yamkini likawa na agenda za kisiasa. Hali ya kutaka kuwagawa wakristo inafanywa na baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo. Hayo yalijitokeza mara nyingi kwa njia tofauti hadi kutaka kuleta utengano miongoni mwa waumini wao wanachama wa vyama mbalimbali vya kisiasa. Mtu anaweza kuhoji majukumu na wajibu wa viongozi wa Kanisa Katoriki nchini Burundi! Mwenendo huo ni hatari, tunaomba viongozin hao wabadili tabia na watambue kwamba kazi zao ni kulinda na kuokoa roho za wakriso wote ;
6. Tukirejea mashimo katika mitaa ya wahalifu walimozikwa watu, yaliyoonyeshwa na vijana magaidi waliojisalimisha baada ya kupuuza itikadi ya wafadhili wa mtandao; yanadhihirisha uhusika wa Paul Kagame katika kuvuruga amani ya Burundi kwa kuwapa silaha waasi na kuwawezesha wahusika. Kwa kuzingatia yaliyotajwa hapo juu, chama CNDD-FDD kinaona kuwa Paul Kagame na Louis Michel wanapaswa kuwajibika kwa maovu dhidi ya binadamu na uharibifu wa mali. Pia wajibu hoja za mashimo walimozikwa watu, ugaidi, utekaji nyara wanachama (Abagumyabanga) na wapenzi wa chama, kusingizia uongozi wa nchi tuhuma za mauaji, na kuandaa mauaji ya halaiki kama ambavyo ukweli umedhihirishwa. Ni wazi tuhuma hizo ziko upande wao ;
7. Chama CNDD-FDD kilitaarifu Jumuiya za Kitaifa na Kimataifa watu wote waliofanya maovu yaliyoisibu nchi tangu uhuru. Chama pia kilionyesha uhusika wa baadhi ya mashirika ya Kimataifa na nchi kadhaa katika mipango ya kuondoa kwa nguvu uongozi unaochaguliwa na wananchi tangu uhuru hadi sasa. Ilitajwa kuwa yapo makundi ya warundi waliopoteza utu ambao daima hutaka kusambaratisha uongozi wasiopenda. Wakati wote nguvu za nje na mashirika ya habari vilitumiwa ili kuficha ukweli, hivi sasa siyo rahisi kwani walioandaa vurugu tangu tarehe 26 Aprili 2015 walionyesha wenyewe jinsi mipango ilivyoandaliwa. Wahusika hao wameanza kupiga kelele za hofu kama watoto na kuandika mengi kwa kujitetea kuwa hawamo, lakini itawagharimu miaka mingi kujinasua. Wajue kwamba siyo maelezo yao yatakayowatakasa. Chama CNDD-FDD hakioni uzito wa maelezo ya watuhumiwa wa maovu, kama ambavyo wahenga walisema : « Kujitetea mara nyingi ni mbinu ya kuficha ukweli » Kwa nini wahangaike ? Tunadhani watulie tu, wakubali yaishe!;
8. Kuhusu mazungumzo ya warundi, tukirejea ushuhuda wa walionyosha mikono kutoka makundi ya wahalifu, chama CNDD-FDD kina msingi na hoja za kukataa kuzungumza na magaidi na waliotaka kupindua uongozi uliochaguliwa, pia msimamo huo hautabadilika kwa sababu zifuatazo :
– Kama ilivyo hata Ulaya, zingatia yaliyotokea Ubelgiji tarehe 22 Machi 2016, gaidi yeyote anapaswa kupigwa vita na wote popote pale ;
– Na kuwa waliosababisha mauaji ya tangu tarehe 26 Aprili 2015 si wanasiasa wenye nia njema bali ni wauaji kwa ushahidi wa mashimo walimozikwa watu wengi wasio na hatia, kuharibu mali za watu, kufanya mauaji ya halaiki kama ambavyo hivi karibuni tarehe 22 Machi 2016, wameua maafisa wawili wa jeshi la ulinzi Kanali Luteni Darius Ikurakure na Meja Didier Muhimpundu pamoja na askari polisi Dieudonne Nsengiyumva aliyetekwa nyara, wote hao bila visa vya kisiasa. Huo ni ugaidi kama unaotokea Ulaya mfano Ubelgiji na penginepo ;
9. Wakati wote wa uchaguzi kwa kuzingatia Katiba na sheria nyingine kama ilivyo hadi leo, yalitokea mauaji yakiwemo ya halaiki. Ajabu ni kwamba wahusika wanatumia staili ile ile kana kwamba mambo hayajabadilika katika fikra zao, huku wakisahau kuwa kila kukicha wananchi wanapiga hatua katika siasa na uhuru wao. Yaliyokuwa sirini sasa yako wazi! Mwaka 1961, 1965, 1972-73, 1988 na 1993 kuna mauaji yaliyofanyika kisirisiri na wahusika wa maovu hayo wasijulikane. Lakini tangu mwaka 2005 wameyafanya hadharani. Siku hizi waandaji wa maovu hujikuta wamejulikana na kuonekana utadhani ni mchezo wa filamu. Hivyo hawana nafasi katika mazungumzo ;
10. Chama CNDD-FDD kinahitimisha tangazo hili kwa kuomba watenda maovu wajirudi, warejee zizini na kuomba msamaha. Kubaki katika mienendo hiyo ya aibu ni kutojipenda na kujivua utu na ubinadamu. Mwanaume hukiri makosa ili asionekane mbele ya waliopo na waliokufa kama laana na msaliti. Kutokana na hayo, chama CNDD-FDD kinawatolea wito warundi wote wa ndani na nje wasiobanwa na Azimio No 2248 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kushiriki Mazungumzo wakiwa na moyo wa uzalendo wa kusema ukweli kwa maslahi ya Taifa, ikizingatiwa kuwa si Mazungumzo ya watu wa Ulaya, kwani hakuna cha kugawana. Ni mwaliko usiobagua wala kumtenga mdau yeyote, hii itasaidia nchi kupiga hatua mbele zaidi na kuandaa mipango yake vizuri, hasahasa ya uchaguzi.

Imetolewa Bujumbura, tarehe 26 Machi , 2016
na Mwenyekiti wa chama CNDD-FDD

Mbunge, Pascal Nyabenda

29 mars 2016

About Author

Evelyne


Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *