Tangazo

TANGAZO No 45/2015 LA CHAMA CNDD-FDD LA TAREHE 23 DESEMBA 2015

Louis Michel na washirika wake wanaunga mkono kubadilishana madaraka kikabila na ndio washauri wa propaganda wa waliokamatwa na vipeperushi mkoani Karusi    

     21 Desemba 2015 kuwa kabila moja liangamize jingine.

  1. Mnamo tarehe 17/12/2015 yalitokea mambo ya kustaajabisha pale ambapo Mbelgji Louis Michel akishirikiana mazungumzo na Marguerite Barankitse katika nyumba za Louvain-La- neuve ambapo watu hao wawili walionyesha chuki kubwa dhidi ya chama CNDD-FDD na serikali yake ya Burundi kuona kwamba inaendelea vizuri. Siyo siri tena tuliyasema tangu zamani kwamba, masuala ya Burundi, mauaji, ugaidi na kupakazia maovu nchi na kuisema vibaya nje na maovu yote yanayotokea nchini yako juu ya Louis Michel na mwanae Charles Michel pamoja na washirika wake. Hayo yana misingi ya mawazo yao ya kuigandamiza nchi tangu zamani. Ni katika azma yao ya kuangusha uongozi uliochaguliwa na wananchi ili hatimaye wamrudishe Petro Buyoya na timu yake ;
  1. Ajabu ni kwamba siku hiyo Louis Michel na Marguerite Barankitse walisema kuwa wanasikitishwa na kushindwa kwa jaribio la mapinduzi la tarehe 13 Mei 2015 lililokuwa na lengo la kuangamiza kabila wasilopenda. Katika mazungumzo hayo walihuzunika kuona kuwa kundi moja la wananchi wakiwemo askari jeshi hawakuunga mkono waliotaka kuiangusha serikali pia kutoungana na magaidi yaliyoshambulia kambi nne za kijeshi hapo tarehe 11 Desemba 2015. Hayo yalisababisha kutofikia azma yao. Ni dhahili hao ndio walioandaa maovu hayo. Waliendelea kusema kuwa wanasikitika kuona Umoja wa Mataifa (UN) na baadhi ya nchi za Afrika wakielewa vizuri masuala ya Burundi na kuunga mkono mamlaka za serikali iliyochaguliwa na wananchi na kuwa karibu kwa kusaidia suala la amani nchini. Ni mengi yanayoonyesha masikitiko yao, hayawezi kuenea katika tangazo hili, hata hivyo baadhi yake hayakuelezwa kwa lugha ya uungwana na ustaarabu ;
  1. Chuki hiyo isiyokoma ya ndugu huyo na wenzake ya kutaka kuangusha Serikali iliyochaguliwa na wananchi kwa vyovyote vile, ili ikiwezekana amrudishe Buyoya na wenzake madarakani hao nao uongozi wao ulitawaliwa na mauaji ya halaiki nchini sawa na ya kimbali ya mwaka 1988 ya Ntega na Marangara. Isingekuwa mchango wa baadhi ya Warundi wapendao nchi waliotangazia mataifa mapema, mauaji ya kimbali yangetokea kama ambavyo kiongozi huyo wa kijeshi alivyokuwa ameandaa. Mwaka 1993 kiongozi huyo wa mabavu aliyekuwa ameshindwa kwenye uchaguzi aliuangusha tena uongozi uliochaguliwa. Wakati huo pia wanasiasa hao wa Ubelgiji waliubariki utawala wake. Naye Mheshimiwa Rais Ndadaye Melchior akauawa bila hata kukemea, yakafuatia mauaji ya wananchi wa makabila yote. Wengine kwa maelfu mwaka 1996 aliwalikusanya pamoja makambini ambapo waliuawa kama inzi. Pia utawala wa Ubelgiji walikuwepo na hakuna aliyefika Burundi kutoa pole. Ingawa mambo hayakuwekwa wazi, chama CNDD-FDD kinaona kwamba yalikuwa maandalizi ya mauaji ya kimbali ya Buyoya na wenzake . Haishangazi sasa kusikia wakati Louis Michel na Marguerite Barankitse waliposema kuwa mauaji ya kimbali yameanza nchi Burundi, Buyoya naye alithibitisha kuwa mauaji hayo yanaweza kutokea wakati wowote. Tujulishe kwamba kata za jiji la Bujumbura za Mutakura, Cibitoke, Nyakabiga, Musaga, Ngagara na Jabe daima zilikuwa zikimtii Petro Buyoya alipokuwa madarakani na hadi leo ni washirika wake muhimu ambao baada ya 1993 waliunda makundi ya vijana wa sans échecs na sans défaites hao walianzisha vurugu katika jiji la Bujumbura na kusimamisha shughuli zote pamoja na kuuwa watu katika kata za Kamenge na Kinama ;
  1. Lugha ya mauaji ya kimbali nchini Burundi huwa inatajwa na maadui wa demokrasi. Ilidhihirika katika mashambulizi ya tarehe 11 Desemba, 2015 ambapo magaidi walipokuwa wakipanga kushambulia makambi ya kijeshi, wapo watu hapa nchini na nje ya nchi hususan waandishi wa habari waliopoteza maadili ya kazi yao waliosema kuwa mauaji ya kimbali yameanza. Ina maana kwamba kama kambi hizo zingetekwa wangetekeleza mpango wa mauaji kama walivyokuwa wameandaa. Kuwa haikuwezekana hayo yanamkasirisha Louis Michel kama alivyosema katika mazungumzo yake. Wazo hilo la mauaji ya kimbali linarejelewa pia na Rufyiri kwa kile alichokiita : » kubadilishana madaraka kwa misingi ya kikabila ». Kuna habari walizopeana wanaounga mkono mawazo ya Rufyiri kupitia mitandao ya kijamii kuwa kama kabila la kina Rufyiri lingefikia uongozi, baada ya miaka mitano wangebadili sheria na kuangamiza kabila wasilotaka, hatimaye kabila hilo lisirudi tena madarakani. Ujumbe huo wa maandishi unadhihirisha mawazo ya kikoloni ya Louis Michel. Hayo ndiyo Chama CNDD-FDD na serikali yake kinapiga vita ;
  1. Hivi karibuni tarehe 21 Desemba, 2015 ametokea mtu mmoja huko Karusi aliyekamatwa na vipeperushi vya maandishi yasiyo na saini. Vipeperushi hivyo vina maandishi yanayowatolea wito kabila la wahutu kuwaangamiza watutsi eti kama ilivyofanyika tarehe 11 Novemba, 2015 katika baadhi ya kata za jiji la Bujumbura. Kitu cha ajabu aliyekamatwa na vikaratasi hivyo ni mtutsi anaye watolea wito wahutu kuangamiza watutsi. Hiyo inaonyesha roho mbaya ya wanaowatuma na kuwapa pesa na silaha ili kuisambaratisha nchi, akina Louis Michel, Charles Michel, Petro Buyoya, Marguerite Barankitse na wengineo ambao hatimaye hufurahi na kusema kuwa tulichotaka tangu awali ni hicho ;
  1. Chama CNDD-FDD kinaona kuwa yawe mawazo ya uongozi kwa kubadilishana kikabila, vipeperushi vya kutolea wito watu kumalizana, yawe mazungumzo ya Louis Michel na Marguerite Barankitse , hata yanayosemwa ya mauaji ya kimbali, mauaji na ugaidi pamoja na kushambulia kambi za kijeshi yote yanalenga njia moja :
  • Kuichafua serikali iliyochaguliwa na wananchi na kuizushia mabaya ili wananchi wagawanyike,waichukie serikali yao, pia uongozi uchukiwe katika mataifa hivyo nchi ibaki bila kuungwa mkono,
  • Kuangusha uongozi wa nchi kwa kutumia nguvu za kijeshi za makundi tofauti na maandamano haramu ya baadhi ya wanachi,
  • Mwisho, waandalizi wa maovu hayo waiweke serikali dhalimu watakayounga mkono na kurejesha nyuma nchi ya Burundi katika hali ya ukoloni wa Ubelgiji tulioupinga tulipojipatia uhuru. Hayo yamebainika, sasa yako wazi na chama CNDD-FDD kitayapiga vita kwa nguvu zote, wakati wote wa uhai wake ;
  1. Chama CNDD-FDD kinahitimisha kwa kuwatolea shukrani za dhati wananchi wote kwa kuendeleza mshikamano ingawa adui alitaka kuwagawa katika makundi akashindwa. Chama kinawaomba kuendelea na msimamo huo kwani adui bado yupo. Chama pia kinawashukuru na kuwapongeza sana mamlaka za ulinzi na usalama kwa umoja wao na kusimamia kikamilifu taasisi zote za uongozi wa Taifa na wananchi kwa ujumla, ingawa yamkini huyu au yule yaweza kuwa amepotoka kutokana na yanayosemwa. Adui alishaona kuwa amebainika na zaidi ya hayo wananchi walimuonyesha kuwa wanachokipenda ndiyo mapenzi ya Mungu. Kwa dhati, kutoka moyoni, chama kinawashukuru Umoja wa Mataifa (UN) na nchi marafiki walioendelea kutambua vizuri suala la Burundi na kuichukulia nchi na wananchi wake maamuzi mazuri. Pia chama kinayashukuru mashirika ya kikanda ambayo Burundi ni mwanachama yaliyoendelea kuiunga mkono nchi ya Burundi katika kipindi hiki kigumu. Mashirika hayo yanaombwa kuendelea kuunga mkono wananchi katika vita vya kupigania na kulinda uhuru wao. Lakini chama hakisahau kutamka kuwa kuna asasi moja ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa inayoongozwa na Kamishna mkuu Zeid Ra’ ad Al Hussein ambaye hakuchoka kuuchafua Umoja wa vijana wa chama CNDD-FDD (Imbonerakure) kwa unafiki wake na uongo mwingi alipowafananisha vijana hao na makundi ya kigaidi. Huyo naye anaudhalilisha Umoja wa Mataifa( UN).

Tangazo limetolewa Bujumbura, tarehe 14 Desemba, 2015

Mbunge Pascal Nyabenda

Mwenyekiti wa Chama CNDD-FDD

24 décembre 2015

About Author

Willy


Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *