Tangazo

Salamu za rambirambi kwa nchi ya Ufaransa na watu wake.

TANGAZO N° 41/2015 LA CHAMA CNDD-FDD LA TAREHE 16 NOVEMBA, 2015.

  1. Baada ya kusikia mashambulizi ya kigaidi katika nchi ya Ufaransa, chama CNDD-FDD kinatoa salamu zake za rambirambi kwa Ufaransa na watu wake. Chama kinasikitishwa na uhalifu na kulaani kwa nguvu zote ugaidi huo usiobagua nchi au sehemu yoyote ya dunia. Ni wakati ambapo nchi zote za Ulimwenguku kuungana na kupiga vita ugaidi huo popote;
  1. Chama CNDD-FDD kinaona kuwa magaidi wote duniani wanafanana kwa matendo yao ; kuua bila kuuliza chochote wala kueleza sababu za mauaji hayo. Ugaidi huo huonekana katika Afrika, Ulaya na kote duniani. Hakuna magaidi maalum na wa pekee kwa nchi fulani, wanapaswa kupigwa vita kwa njia na mbinu moja ;
  1. Chama CNDD-FDD kinaungana na Ufaransa na watu wake katika huzuni za msiba huo mkubwa uliowafikia. Burundi na wananchi wake imeguswa na msiba huo kama ilivyowagusa Wafaransa ;
  1. Chama CNDD-FDD kinaamini bila shaka kuwa wananchi wa Ufaransa wataweza kushinda uovu huo kama inavyoonyesha katika historia yao kuwa wana nguvu pia hawachoki ;
  1. Chama CNDD-FDD kinahitimisha salamu hizi za pole kwa kumuomba Mungu kuilinda Ufaransa na watu wake na kuomba mataifa mengine kuwa karibu na Wafaransa kwa misaada kwani rafiki wa kweli huonekana wakati wa shida.

 

Tangazo limetolewa Bujumbura, tarehe 16 Novemba, 2015.

na Mheshimiwa Mbunge Pascal NYABENDA,

Mwenyekiti wa Chama CNDD-FDD.

16 novembre 2015

About Author

Willy


Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *