Tangazo

TANGAZO N° 036/2015 LA CHAMA CNDD-FDD LA TAREHE 15 Septemba, 2015

WANAOUA WATU HAWAJUI WANACHOKIFANYA, WANA KIU YA DAMU TU


Wanasiasa wa upinzani sugu wasiopenda kuutambua uongozi uliopo wamechagua njia isiyofika. Kumekuwepo na mauaji ya kupanga yakilenga baadhi ya viongozi ambao ni  maafisa katika mamlaka za ulinzi na walio katika vyama vya upinzani. Mifano ni kuuawa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama UPD – Zigamibanga Zedi Feruzi, mwezi Mei, 2015.  Julai wauaji walimjeruhi Lt Col. SINDAYE Dismas kamanda wa kikosi cha ulinzi kwenye Radio na Televisheni ya Taifa . Kifo cha Lt General Adolphe NSHIMIRIMANA katika shambulio, walifariki pia polisi walinzi wake wawili (2) hapo mwezi Agosti 2, 2015 ; wauaji walitumia roketi na silaha nzito nzito,  na mwezi Agosti 15, 2015 aliuawa afisa mstaafu aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi Col BIKOMAGU Jean.
Tarehe 7 Septemba, 2015 aliuawa Patrice GAHUNGU aliyekuwa msemaji wa UPD –Zigamibanga ; Septemba 11, 2015 Mkuu wa majeshi ya Taifa Major General Prime Niyongabo alinusurika kifo katika shambulizi la kuvizia la  silaha zikiwemo roketi ; shambulio hilo liligharimu maisha ya walinzi wa General watatu na wawili kati ya washambulizi hao wauaji.

  1. Chama CNDD-FDD kinalaani kwa nguvu zote mauaji hayo yasiyo na maana ambayo yanatafsiri kwamba wauaji hao hawana lolote la kuwasaidia warundi bali umwagaji wa damu na kutia hofu. Siasa ya kuuwa haina nafasi tena katika uongozi wa demokrasi ;
  1. Chama CNDD-FDD kinaungana na wote wanaofiwa na ndugu na jamaa zao wa mamlaka za ulinzi na usalama pamoja na wanachama (Abagumyabanga) wanaopoteza maisha kwa sababu tu ya kupigania  amani na usalama na kuimarisha umoja wa Warundi. Chama kinatumia fursa hii kumuunga mkono na kumtia moyo Shujaa General Prime NIYONGABO Mkuu wa majeshi katika majukumu yake na kumshukuru Mungu kwa kunusurika kifo hapo tarehe 11 Septemba 2015 ;
  1.  Chama CNDD-FDD kinaomba kwa dhati kuwa hao wanaoandaa mauaji hayo popote walipo wakamatwe na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Aidha serikali inaombwa kutumia polisi wa kimataifa ili isaidie kusaka na kukamatwa kwa wauaji hao.
  1. Chama CNDD-FDD kinawakumbusha wanasiasa sugu na washirika wao na wanaowaunga mkono kusimamisha mara moja mauaji hayo yanayo walenga baadhi ya watu kwani kazi ya kujitoa mhanga haisahauliki, ni sawa na mauaji ya kimbali. Mazungumzo hayawezi kufuta kamwe maovu au mauaji ya kimbari yanayotendwa;
  1. Chama CNDD-FDD kinahitimisha kwa kuwatolea wito warundi wote kwa namna ya pekee wanachama ( Abagumyabanga) kuwa macho, wasikate tamaa bali waendeleze umoja na mshikamano kwani adui anatafuta njia ya kupitia ili akisambaratishe chama CNDD-FDD na taifa kwa ujumla.Tunaomba  wahisani na  Jumuiya ya Kimataifa kusitisha hatua ya kutoisaidia Burundi katika miradi ya maendeleo iliyoandaliwa kwa nchi ya Burundi kwani Serikali inayojumuisha makundi yote inatimiza wajibu wake hivyo msaada ni muhimu. Na hakuna yeyote duniani awezaye kuunga mkono mauaji yanayobagua watu katika nchi.

  Tangazo limetolewa Bujumbura, tarehe 15 Septemba, 2015.

  na  Mheshimiwa Mbunge Pascal NYABENDA,

  Mwenyekiti wa Chama CNDD-FDD. 

15 septembre 2015

About Author

Willy


Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *