Tangazo

TANGAZO No 001 /2016 LA CHAMA CNDD-FDD LA TAREHE 05 JANUARI 2016

MWANZO WA MCHAKATO WA MAZUNGUMZO YA WARUNDI YALIYOANZA TAREHE 28 DESEMBA, 2015 ENTEBE KATIKA JAMHURI YA UGANDA.

  1. Tarehe 28 Desemba, 2015 Entebe nchini Uganda zilifanyika sherehe za uzinduzi rasmi wa mazungumzo ya warundi chini ya mpatanishi Mheshimiwa YOWERI KAGUTA Museveni Rais wa Uganda ;
  2. Walioalikwa na kuhudhuria katika uzinduzi huo ni wawakilishi wa serikali ya Burundi na wa chama CNDD-FDD, baadhi ya wanasiasa wa sera mbadala waumini wa demokrasi pamoja na wapinzani sugu wenye misimamo mikali na waliofanya jaribio la mapinduzi wakiwa na baadhi ya wanahabari waliopoteza maadili ya kazi yao, baadhi ya asasi za kiraia na viongozi wa kidini ambao walikuwa karibu kwa njia moja au nyingine katika maandamano haramu ya umwagaji wa damu, hali iliyoanza tangu 26 April, 2015 nchini Burundi. Zaidi ya hao, walialikwa pia wawakilishi muhimu wa kidiplomasia na wajumbe wa Jumuiya mbalimbali za Kimataifa na Mashirika kadhaa bila kusahau wajumbe waliowakilisha Jumuiya za kikanda ambazo Burundi ni mwananchama wake ;
  1. Chama CNDD-FDD kinatumia fursa hii kumshukuru Mheshimiwa YOWERI KAGUTA Museveni ambaye pamoja na majukumu yake ya kipindi hiki yanayoambatana na kampeni za uchaguzi nchini mwake, akiwa mmoja wa wagombea kiti cha urais, aliweza yeye binafsi kuzindua mazungumzo hayo yaliyotajwa ;
  2. Daima mwanzo ni mgumu na huwa na matatizo ya kipee, hivyo siyo rahisi kuweka mambo sawa kwa wakati na kumridhisha kila mmoja. Chama CNDD-FDD kinaona kuwa kuna haja ya Serikali ya Burundi kuzungumza na msuluhishi kuhusu kasoro zilizojitokeza katika maandalizi ya uzinduzi wa mazungumzo, ili kuweka utaratibu mzuri wenye malengo sahihi katika mchakato wa mazungumzo hayo ya warundi kwa azma ya kufikia matarajio bila vipingamizi. Chama kitafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa mazungumzo hayo yanawafikisha warundi kwenye maamuzi na mwafaka wa kudumu kwa kuheshimu demokrasi kulingana na wakati huu; huku tukijiepusha na mienendo ya mazungumzo ya Arusha kati ya makundi ya wanasiasa waliokuwa na tamaa ya kugawana madaraka ; badala ya mazungumzo ya kujumuisha wananchi wote wao wenye madaraka ya uongozi. Hii inabainisha ukweli kwamba ile Kamati ya Mazungumzo ya Warundi CNDI inapaswa kuchukuwa nafasi muhimu ya kuwasikiliza wananchi wote bila ubaguzi. Hivyo ni mwiko kubatilisha matokeo ya uamuzi uliofanywa na wananchi katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2015 ;
  3. Chama CNDD-FDD kinampongeza Msuluhishi kwa msimamo wake wa kuheshimu na kuzingatia yaliyomo katika Azimio No 2248 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN la tarehe 12 Novemba, Mwafaka wa Mazungumzo ya Amani ya Arusha, Katiba ya Nchi ya Burundi na kutaja matatizo nyeti ya warundi ambayo baadhi hawapendi yaelezwe bayana : ( Kuamini mwenendo wa demokrasi unaompa mtu yeyote haki ya kuwa katika amani ). Lakini sasa haifahamiki vizuri sababu ya Mpatanishi kukiuka maazimio kwa kuwaalika waliotaka kuangusha uongozi uliochaguliwa na wananchi hapo tarehe 13 Mei, 2015 na kuendelea. Ingawa ni hivyo, Mpatanishi alisikia mawazo ya baadhi ya wanaotaka kubadilishana madaraka kikabila na wenye hofu kuwa walio wachache hawawezi kurudi tena madarakani kwa njia ya uchaguzi wa demokrasi, hii ina maana nia yao ni kufikia madaraka kwa njia ya mapinduzi kwa kutumia nguvu na ugaidi, kama tulivyoyaona mwaka jana, wapo pia wanaodai kuwa kama siyo wao bora nchi ifutike. Hivyo ndivyo matatizo ya Burundi yalivyodhihirika. Kama wahenga walivyosema : « Jiwe lilojitokeza halidhuru jembe » ;
  4. Chama CNDD-FDD daima kinahoji kwa nini hutokea taharuki na uhasama hapa nchini kabla na baada ya uchaguzi? Hadi kusababisha vifo vya wananchi wasio na hatia! Mwaka 1961 shujaa na mhanga wa uhuru, Mfalme Louis Rwagasore aliuwawa yeye na familia yake mara baada ya uchaguzi; ambapo Chama cha UPRONA kulikuwa kimeshinda katika uchaguzi huo. Kwa nini mhanga huyo aliuawa?. Mwaka 1965, Waziri Mkuu wa kwanza Pierre Ngendandumwe ambaye alikuwa kama kiongozi wa pili katika chama cha UPRONA mwaka 1961 baada ya RWAGASORE, naye pia aliuawa akifuatiwa na halaiki ya waliomuunga mkono katika chama cha UPRONA. Hayo yalisababishwa na nini? Mnamo mwaka1993, Mheshimiwa Ndadaye Melchior, mhutu wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasi na Mhanga wa Demokrasi ilikuwa zamu yake, aliuwawa pamoja na maelfu ya raia wapenzi wa demokrasi mataifa yakishuhudia bila kukemea. Walionusulika katika mauaji hayo waliwekwa pamoja kwenye kambi za mauaji ya kimbali kama zile za Nazis au za maangamizo ambapo wananchi zaidi ya laki tano (500.000) waliuawa hovyo sababu ya ukosefu wa mahitaji muhimu ya maji na chakula. Katika 1996, wakimbizi wa Burundi wapatao 5,000 walifukuzwa na ujio wa FPR-Inkotanyi katika bonde la Rusizi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo(DRC). Wakimbizi hao waliuwawa na FPR-Inkotanyi wakati wakielekea mji wa Shabunda; maiti walitupwa katika mto kando ya mji huo. Bill Clinton Rais wa Marekani wa chama cha Demokrasia wakati ule hakutoa kauli yoyote, kama hakulaani maovu hayo. Je, hayo yote ilikuwa awamu ya tatu au kulikuwa na agenda ya siri? Mfululizo wa mapinduzi ya serikali  yalitokea nchini lakini Mataifa yalikaa kimya kwani walijua mipango hiyo miovu. Mwaka 2015, baadhi ya nchi katika mataifa walitumia mbinu na ujanja ili waweze kubadili hali ya mambo iwe kama wanavyopenda na kuangamiza wananchi wanaounga mkono uongozi wa kidemokrasi ; ikiwezekana waweke madarakani wanaowataka. Mungu pekee ndiye ajuaye hatma ya mipango hiyo ya kishetani dhidi ya warundi. Mpatanishi katika mazungumzo hayo bado ana kazi kubwa, kwani anapaswa kutoa uhuru kwa warundi kujua chimbuko la maovu yote hayo na nafasi/ushiriki wa kila mmoja katika yote yaliotajwa. Chama CNDD-FDD kinapenda kumjulisha tena Mpatanishi kuwa kinaunga mkono kufanyika kwa  mazungumzo hayo nchini Burundi na nje ya nchi. Hii ina maana kwamba CNDI na mpatanishi wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na uwazi pamoja na kuafikiana mawazo ;
  5. Chama CNDD-FDD kinaamini kuwa muda umefika kwa warundi kurejea na kukumbuka historia yao ingawa haipendezi, kutokana na matatizo ambayo yamekuwa yakiwafikia. Ufanyike utafiti na uchunguzi wa kina kwa utulivu na uhuru wakati wote itakapolazimu, ili ukweli kwa yaliyoisibu nchi udhihirike, hatimaye kufikia demokrasi iletayo amani kwa wote. Si rahisi watu kuamini mwenendo wa demokrasi na kuondoa hofu  ya kuzungumza bayana kwa uwazi na uhuru. Kuna haja ya watu kupata faraja na kujua thamani ya mwananchi kujichagulia viongozi na kwamba njia ya demokrasi inaheshimu na kulinda haki ya wote. Si katika mazungumzo yanayokutanisha wawakilishi wapatao hamsini hivi ambapo ufumbuzi wa kudumu wa migogoro ya Burundi utapatikana. Mheshimiwa YOWERI KAGUTA Museveni majukumu yenu si mepesi, umakini na maarifa vinatakiwa; kwani kazi ya usuluhishi inayofanyika nje ya nchi ikumbuke kuwa kuna matarajio ya warundi wengi wenye mchango katika mazungumzo hayo. Chama CNDD-FDD kinaomba utaalamu, ujuzi na maarifa vitumike na Kamati ya Mazungumzo ya Warundi ufanye kazi yake kwa bidii kote nchini na kuwafikia walio nje ya nchi ili asitengwe au kubaguliwa hata mmoja. Chama CNDD-FDD kinatumia nafasi hii kumtakia Mpatanishi ufanisi na mafanikio katika majukumu hayo pamoja na kumtakia mema na heri ya mwaka mpya wa

Tangazo limetolewa Bujumbura, tarehe 05 Januari, 2016

na   Mbunge Pascal Nyabenda

Mwenyekiti wa Chama CNDD-FDD

6 janvier 2016

About Author

Willy


Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *