Tangazo

TANGAZO N° 003/2016 LA CHAMA CNDD-FDD LA TAREHE 17 FEBRUARI, 2016.

Wanaokalia fikra za mauaji ya halaiki na mashimo walipozikwa watu wengi kwa pamoja, ndio hao wasiokubali Mazungumzo ya Warundi na ile Kamati ya Ukweli na Maridhiano ya Warundi (CVR)

1. Katika mwaka 1959, baada ya kushindwa kuangusha utawala wa wakati ule nchini Rwanda, kuna baadhi ya Wanyarwanda walikimbilia nchini Burundi na kupewa hifadhi ya ukimbizi. Hakuna ubaya wa kukimbia nchi, kwani hayo humfikia yeyote yule hapa duniani .Mara baada ya kufika Burundi walipokelewa kwa moyo mkujufu, lakini tatizo ni kwamba baada ya kupatiwa mahitaji yote muhimu, wakimbizi hao walianza kuunda propaganda na mbinu za uongo kwamba kabila lililo dogo hapa Burundi linaweza kufikiwa na mauaji ya halaiki kama ilivyokuwa imetokea kwa ndugu zao wa Rwanda. Polepole viongozi wa Burundi wa wakati ule na miaka iliyofuata walianza kuandaa namna watakavyofanya mauaji ya kimbali mapema ili kuwahi kama walivyokuwa wameshauriwa na hao wakimbizi wa Rwanda. Propaganda hizo za uongo wa hao wageni ziligharimu uhai wa Mfalme Louis Rwagasore mwaka 1961 na kifo cha Waziri Mkuu Petro Ngendandumwe na halaiki ya watu wengi mwaka 1965 pamoja na mauaji ya kimbali ya mwaka 1972. Mauaji mengine ya halaiki yanayojulikana ni ya baada ya mwaka wa sabini hadi sasa ; yaliendelea kuwa na uhusiano zaidi na uongo wa baadhi ya viongozi wa wakimbizi wa Kinyarwanda ;

2. Ikumbukwe kuwa katika mauaji hayo ya maangamizo nchini Burundi, wamo warundi na wageni. Hao wanajiunga kwa pamoja na kujificha wakati wote ili sheria isichukue mkono wake dhidi yao. Ndiyo maana makundi haya ziku zote tunayaita makundi ya wanasiasa magaidi ambao daima hutaka kuangusha viongozi waliochaguliwa kidemokrasi. Wanasababisha umwagaji damu na kuua watu ili kufumba macho ya Warundi na Mataifa kama njia ya kuzuia watuhumiwa wa maovu hayo wasijulikane. Hao ndio wanashinda kutwa katika maabara ya hila na uongo wakipika mawazo ya mauaji na namna ya kujitua mizigo ya maovu waliyowatendea warundi. Wanabebesha mabaya wanayotenda na wanayoendelea kufanya kwa chama CNDD-FDD na serikali yake. Chama CNDD-FDD kinakumbusha mauaji ya kimbali yaliyofanywa na Michel Micombero (Génocide physique), mauaji ya viongozi na wasomi (Génocide intellectuel) ya Jean Baptiste Bagaza na mauaji ya demokrasi (Génocide démocratique) ya Petro Buyoya. Wakati wote huo kilikuwa kipindi cha mateso ya kisiasa nchini Burundi. Wapo baadhi ya wakimbizi wa kinyarwanda waliopewa hifadhi hapa nchini waliojihusisha kwa njia moja au nyingine katika kuandaa na kutekeleza maovu hayo ya kishetani. Watu hao ndio hawataki kusikia au kuwepo mazungumzo ya warundi (CNDI) au ile Kamati ya Ukweli na Maridhiano (CVR), kwani wanajua mwishowe yatadhihirika ;

3. Kwa hiyo haishangazi kusikia kuwa Paul Kagame bingwa na mtaalam wa mawazo na mipango ya mauaji ya halaiki katika kanda kama alivyoyafanya kwake, akitaka kuyaingiza nchini Burundi kupitia makundi ya baadhi ya warundi waliokimbilia kwake, kwa kuwapa silaha na mafunzo ya kijeshi ili waje wachokoze na kusababisha mauaji ya halaiki katika nchi yao. Ni bahati mbaya kuwa Paul Kagame anasahau methali ya Kirundi isemayo : « Siri ya mtungi aijuaye kata au Akili ni nywele kila mtu ana zake  » . Anadhani kuwa kwa kutumia makundi ya mauaji na ugaidi katika mikoa ya Kayanza na Cibitoke kwa malengo ya kuangamiza wananchi kama alivyofanya kwake mwaka 1994, ambapo aliamuru RPF-Inkotanyi kushambulia wananchi wa Byumba ya wakati ule wapatao 750.000. Wakati wa vita kiasi cha watu wasiozidi laki moja (100.000) walifanikiwa kukimbia, hii ina maana kuwa ambao hawakuponyoka waliuawa. Kwa neema ya Mungu zoezi hilo la aibu na la kusikitisha halikufanikiwa nchini Burundi. Ingawa Petro Buyoya na Louis Michel wako mstari wa mbele wa vinara wa wanaohubiri mauaji ya kimbali ;

4. Mauaji ya kimbali ya wanachi wa Byumba hayakutosha kwani ilipasa kutoa ndugu zake kama kafara kwa kuchokoza taasisi za uongozi wa Rwanda wa wakati ule kupitia maelfu ya vifo kutokana na kujihami kwa upande mwingine. Hayo yaliwezekana nchini Rwanda kwani wananchi walifarakana, lakini Burundi haikuwezekana kwani hata kifo cha Rais Ntaryamira Cyprien hakikusababisha kutengana kwa Warundi. Kitu cha kusikitisha ni kwamba kifo cha Rais Ntaryamira kilitokea alipokuwa akirudi kutoka katika kikao cha Dar-es-Salaam Tanzania katika mazungumzo ya wanyarwanda yaliyokuwa yakiendelea Arusha. Ni bayana kuwa Paul Kagame, Petro Buyoya na washirika wake wenye nia moja kamwe hawataki kusikia habari ya mazungumzo iwe Rwanda hata Burundi. Wanachotaka ni utawala wa mabavu kwa nguvu za jeshi kwa misingi ya kikabila ;

5. Wakati wananchi wa Burundi wanazingatia umuhimu wa Mazungumzo ya Warundi bila ubaguzi kwa kushirikisha warundi wote ili yeyote achangie kwa uhuru na uwazi kuhusu uhai wa nchi hivyo ukweli utawale kwa azma ya kupata ufumbuzi wa migogoro. Baadhi ya Warundi,vibaraka wanaomtii Kagame, wao wanatafuta kuhamishia mazungumzo ya wananchi nje ya nchi ili kuficha ukweli wa historia ya Burundi unaotakiwa kujulikana. Hao wanaweka mbele agenda ya kugawana madaraka katika serikali ya mpito. Kwa unafiki, wanadai kutetea Katiba ya Nchi na Mwafaka wa Arusha, wakati haja yao ni uchu wa kutaka kujinufaisha kupitia nyaraka hizo kwani wanatafuta mwafaka mwingine unaofanana na ule wa Arusha. Chama CNDD-FDD na serikali yake ndivyo pekee vyenye wajibu wa kusimamia na kutetea Mwafaka wa Arusha ;

6. Baada ya kupoteza nguvu katika uga wa kisiasa na vyombo vya habari kuhusu mawazo yao ya kuletwa vikosi vya Kimataifa MAPROBU, na kuona kuwa wananchi wa Burundi wanakataa na kupinga mawazo ya mauaji ya kimbali yaliyopandikizwa na maadui wa nchi, wamejikuta njia panda ndiyo maana wanakataa mazungumzo ya Burundi yanayoweka wazi ukweli kwani maovu na uhalifu wao vitabainika. Maadui wa Amani na Utulivu wa nchi wakisaidiwa na vijana wao waliofundishwa ugaidi nchini Rwanda, wakizidisha uvumi na uongo walifanikiwa kuhadaa Jumuiya ya Kimataifa eti kuna « mashimo mapya walimozikwa watu wengi » nchini Burundi na kwamba Umoja wa Mataifa unapaswa kuagiza kamati ya uchunguzi. Lakini yote yana lengo la kutaka kuvunja nguvu za chama CNDD-FDD na serikali yake hivyo ikiwezekana iwekwe serikali ya mpito ;

7. Kama chama CNDD-FDD kilivyosema awali katika tangazo lake No 002 la tarehe 05 Februari, 2016. Burundi ni nchi huru inayojitawala. Wananchi wa Burundi wanashukuru tena Umoja wa Mataifa (UN) kwani katika Maazimio yake No 2248 ya tarehe 12 Novemba, 2015 uliagiza kuwa uhuru wa Burundi uheshimiwe na mipaka yake pamoja na Umoja wa Warundi. Chama CNDD-FDD kinaomba Umoja wa Mataifa kuheshimu na kutambua Kamati ya Ukweli na Maridhiano ambayo tayari iko kazini ili iainishe maovu yote yaliyoisibu nchi tangu uhuru wake hadi sasa. Kutuma kamati ya wachunguzi katika nchi bila kupitia Kamati ya Ukweli na Maridhiano (CVR) ni kuficha usoni mwa warundi mipango ambayo imekuwa ikiandaliwa kwani hakujawahi kutokea watalaam wa kuchunguza mashimo walimozikwa watu wengi tangu nchi ilipopata uhuru. Hata kaburi alimozikwa Mfalme Ntare V, Karoli Ndizeye haijulikani ilipo, wananchi wanatamani kupajua. Umoja wa Mataifa (UN) haujafanya lolote kuhusu hilo pia akina Buyoya, Bagaza na washirika wao hawataki kusema au kuonyesha alipozikwa. Wakati mkoloni Louis Michel na washirika wake wanadai kuelewa vizuri historia ya Burundi, hata Ubelgiji waliyofanya chochote walichotaka wakati wa ukoloni nchini Burundi, kwa nini hawataki kuonyesha alipozikwa Malkia (mke wa Prince Louis Rwagasore mhanga wa uhuru) ;

8. Kama tulivyoeleza mwanzo wa tangazo hili, wanaojishuku au wanaojitambua kuhusika na mauaji yaliyofanyika Burundi wanadhani kuwa ukweli hautawekwa wazi na ndiyo maana wanaendeleza uongo na kuhatarisha amani ya nchi ili kuzuia fursa na nafasi kwa wananchi kutafuta ukweli huo kupitia mazungumzo yasiyobagua. Kuwa walifanya maovu mengi katika historia ya Burundi hadi Kagame kufikia hatua ya kuua Rais Mpendwa wa nchi yetu Ntaryamira Cyprien wasidhani yaliisha kwani wahusika watapaswa kuwajibika. Ukweli unaweza kutatizwa kwa siku moja au mwezi lakini mwisho wake huwekwa hadharani. Si kutaka kutatiza au vikwazo kwa mazungumzo ya warundi wala kutaka kupindua serikali kupitia mazungumzo ya baadhi ya mataifa ya Ulaya yenye lengo la kuzaliwa serikali ya mpito vitakavyozuia kujulikana kwa ukweli wa Burundi. Njia hiyo haifiki, wajue kwamba : « Kila lenye mwanzo lina mwisho  » ;

9. Chama CNDD-FDD kinahitisha tangazo hili kwa kuwataka utulivu wananchi na kuendelea kushikamana, na kushiriki mazungumzo ya Warundi kwani ukweli ni tiba ya uhasama. Chama CNDD-FDD kinaomba Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kuunga mkono na kuiwezesha kipesa Kamati ya Mazungumzo (CNDI) ili iweze kwenda kusikiliza warundi walio nje ya nchi, hatimaye ripoti yake iwe na mawazo ya warundi wote.

Imetolewa Bujumbura, tarehe 17 Februari, 2016
Mwenyekiti wa chama CNDD-FDD
Mheshimiwa Pascal Nyabenda

18 février 2016

About Author

Evelyne


Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *