Jumuiya ya nchi za Ulaya imechukulia baadhi ya warundi hatua za uchokozi zisizofariji kinyume na sheria
Tarehe 01 Oktoba, 2015 Jumuiya ya Umoja wa Ulaya ilikutana Ubelgiji ambapo ilichukuwa hatua zisizo wazi na zisizofaa dhidi ya warundi wanne (4) wa kabila moja la wahutu. Hatua hizo zinawakataza watajwa hao kuingia katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo na kuzuia mali zao zinazoweza kuwa katika mataifa hayo 28 yanayounda Jumuiya hiyo.
Chama CNDD-FDD, kilistuka na kushangaa baada ya kusikia hatua hizo; kwa sababu adhabu hizo zinakumbusha historia mbaya ya yaliyoisibu nchi ambapo ubaguzi ulikithiri nchini na umwagaji wa damu uliokuwa ukisababishwa na kundi dogo lililotawala nchi kwa muda wa miaka 40 ukiondoa miezi 3 tu ya uongozi wa hayati Rais Melchior Ndadaye. Kitu cha kusikitisha ni kwamba kila yalipotokea mauaji nchini umoja huo wa nchi za Ulaya walifumba macho na hakuna aliyesimamishwa katika wahusika au kukamatwa na kuchukua hatua kwa maovu ya mipango ya kuangamiza warundi wa kabila moja. Kuna maswali mengi ya kujiuluza. Je, hao hawakuchukuliwa hatua kwa sababu ni washirika wao? Je sheria za wakati ule katika Jumuiya ya Umoja wa Ulaya ni tofauti na sheria za leo ? Je nchi hizo ziliogopa kuchukuwa hatua kwa waovu kwa sababu ni kabila lisiloguswa ? Je watu hao wanne wanaotajwa walifanya yanayofanana na ya wale walioandaa mauaji ya kimbali na kuizushia serikali ? Je hatua hiyo ambayo haikujulishwa serikali ndiyo sheria za Jumuiya ya Ulaya wanazolazimisha mataifa ya Afrika , Caraibe na Pacifique (ACP) kufuata n.k
- Mikutano ya nchi za Afrika , Caraibe na Pacfique (ACP) iliyofanyika Bruseli Ubelgiji kuanzia tarehe 22-27 Septemba, 2015 ambapo agenda ya Burundi ilijadiliwa kwa kurejea tangazo lililoandaliwa na Kamati ya nchi hizo katika Kisiwa cha FIJI katika mji wa Suva mwezi Juni. Wakati wote huo katika vikao vyote hakuna suala la kuwachukulia watu hatua lililojadiliwa. Katika kikao cha mwisho cha Bruseli Ubelgiji kuanzia terehe 22-27 Septemba wawakilishi wa Burundi walionyesha wazi kwamba uchaguzi ulikwenda vizuri, uongozi ukaundwa kwa kuzingatia ushauri wa mataifa ya kikanda, Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika, Umoja wa Nchi za Ulaya, Umoja wa Mataifa na mashirika mbalimbali. Hivyo haieleweki baada ya hapo zije sheria na hatua za ghafla dhidi ya Warundi bila taarifa yoyote kwa serikali ili ifanye lolote au kutoa maelezo.
- Masuala ya siasa yanajibiwa kisiasa na mambo ya sheria yanashughulikiwa kisheria kama ambavyo mahesabu hufuata kanuni zake.
- Adhabu zilizochukuliwa dhidi ya warundi wanne (4) wa kabila moja la wahutu si kwa mujibu wa sheria zinazofahamika duniani ; kwani hakuna sheria zinazolenga kabila moja. Ifahamike wazi hata waliochukuliwa hatua hawakujulishwa ili wajieleze. Yeyote anaweza kufikiria misingi ya hatua hizo kama ilivyotajwa hapo juu. Ni dhahiri kuna kundi la watu lilojiweka juu ya sheria tuzijuavyo na kudanganya watekelezaji wake katika njia zisizofaa kwa kuzingatia kuwa maamuzi yenyewe yalichukuliwa sirini bila serikali kuwepo.
- Kitu kingine cha kushangaza ni namna sheria hizo zilivyochukuliwa kwa lengo la kubomoa mamlaka ya jeshi la polisi. Kwani badala ya kukamata kiongozi mkuu, wanalenga wa chini yake kwa sababu ni mhutu aliyekuwa katika chama CNDD-FDD ;
- Wachunguzi wa mambo wanajua muundo wa Jeshi la Ulinzi na Usalama wa taifa kwa kuzingatia makubaliano ya kusimamisha vita ya tarehe 16 Novemba 2003. Kuchukulia hatua waliokuwa katika chama CNDD-FDD tena wa kabila moja ni dhahiri Jumuiya ya Umoja wa Ulaya walikuwa kinyume na mwafaka huo wa kuleta amani. Ni wazi ingawa NGENDAKUMANA Leonard alikwenda katika wanaoipinga serikali ya Burundi haaminiki katika kuunga mkono kundi hilo la kabila jingine ; kwani hakusema mabaya kuliko yaliyosemwa na Pacifique Ninahazwe, Jenerali Ndayirukiye Cyille, Vital Nshimirimana, Alexis Sinduhije, Marguerite Barankitse na wengineo ;
- Inasikitisha kuona waliotoa amri ya maandamano haramu walitumia watoto katika uovu, kuwapa madawa ya kulevya yote hayo ni kinyume na sheria na haki za binadamu ; baadhi yao walipoteza maisha. Waandaaji wa maandamano hayo bado wanapokelewa na kuhifadhiwa katika nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya. Kuna hoja ya kujiuliza! Hao hao waliwatumia vijana kushambulia warundi wasio na hatia hususan wanachama wa CNDD-FDD (Abagumyabanga) na polisi; wakaua na kuchoma watu na vitu. Wanahabari waliotumwa na nchi hizo walikuwa wakiangalia na kupotosha ukweli wa taarifa ; hupokelewa katika mataifa hayo. Inamaanisha kuwa walishindwa kazi waliyotumwa na kuwarejesha. Na hapa yeyote anaweza kujiuliza kitu ;
- Kutoheshimu vyombo vya sheria (Mahakama ), kuandama baadhi ya watu ili kubomoa mamlaka za polisi zilizowekwa kwa shida huku wakijisahaulisha makosa ya walioandaa maandamo haramu na kutaka kuiangusha serikali, wasitambue wito na nia njema ya serikali na msimamo wake kwa Taifa. Ni dhahiri njia za sheria zinatumika ili kufikia malengo ya kisiasa. Haya ni bayana kwa kuwa sheria zinapindishwa kwa makusudi ili kundi hilo liweze kufikia azma yake.
- Serikali iliyochaguliwa kidemokrasi haina matatizo na yeyote.
- Asasi za kiraia kama vile Initiative et Changement, OLUCOME na mengine, katika mikutano yao na mazungumzo na waandishi wa habari walikuwa wakieleza kuwa maandamano yaliyoambatana na mauaji yaliyokithiri yaligeuka njia ya kutaka kufanya mapinduzi ya serikali iliyochaguliwa na wananchi. Hayo yakifanywa na wanasiasa wa sera mbadala na viongozi wa vyama sugu dhidi ya serikali waliotengeneza uhasama. Ni mawazo ya kuzubaisha watu kwani budi tufahamu kuwa wananchi ndio wenye uwezo wa kuchagua viongozi.
- Kama ambavyo warundi na mataifa ni mashuhuda, maandamano haramu yaliyoambatana na mauaji, yalianza mara tu baada ya wanachama (abagumyabanga) kumteua aliyepeperusha bendera ya chama katika uchaguzi wa Rais Mheshimiwa Petero NKURUNZIZA katika Kongamano la Mkutano Mkuu wa Chama tarehe 25 Aprili 2015. Mkutano huo ulifuatia mikutano ya wanachama iliyafanyika mashinani, tarafani na mikoani kote nchini .Wapinzani kutoridhishwa na uteuzi wa wanachama wa mgombea kiti cha Urais ni kujiaibisha mbele ya umma wapenzi wa demokrasi. Inashangaza sana kwani aliyepitishwa alikuwa wa CNDD-FDD kukiwakilisha chama hicho si vya upinzani. Kwa hiyo madai ya baadhi ya mashirika kwamba hayapiganii maslahi ya kisiasa ni uongo wanaojazwa na viongozi wa vyama wale waliokata tamaa, wasio na sera, wasiopenda kuimarika kwa demokrasi nchini. Kwa upande mwingine vyama hivyo vina matatizo na wananchi kwa sababu ya kuandaa maandamano na vurugu vilivyogharimu maisha ya watu na kuharibu mali za wananchi hadi kutaka kuipindua serikali iliyochaguliwa na wananchi wenyewe.
- Jumuiya ya Umoja wa Ulaya haitaki mazungumzo katika nchi ya Burundi :
- Chama CNDD-FDD kinashangazwa na hatua za uchokozi zilizochukuliwa na mataifa ya Ulaya ya kuwabagua na kuwatenga baadhi ya warundi bila kuwashirikisha au kuwauliza wahusika ; wakati mazungumzo ya wadau wote yakiandaliwa. Kando ya kuwaunga mkono wanaotaka kusambaratisha mamlaka za polisi ambapo hadi leo wameshindwa, nchi hizo zimeamua kuchukua hatua zilizo tofauti na matakwa ya serikali ya Burundi ya kukutanisha warundi wote katika mazungumzo. Wakati huo hakuna wazo jingine jipya mbali na kutatiza mazungumzo kwani waliochukua hatua hawakupata walichodhamiria ambacho ni kuiangusha serikali iliyochaguliwa na wananchi hatimaye uwepo uongozi wa serikali ya mpito ya kugombania madaraka. Ili nchi hizo zipate mwanya wa kuhujumu uchumi wa nchi. Waliokusudiwa kuongoza serikali ya mpito ni dhaifu wasio na uwezo hivyo kufungulia milango washirika wao ;
- Ieleweke wakati mataifa jirani, Jumuiya ya Afrika Mashirika , Umoja wa Afrika, Mashirika ya Kimataifa na Umoja wa Mataifa pamoja na mikutano mingi iliyofanywa ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya Burundi katika mashirika ya Ulaya na penginepo, wote wanakubali kuwa njia ya mazungumzo ni pekee kwa kuleta amani nchini ; mara utasikia hawa na wale wanajitoa katika mchakato wa mazungumzo, badala ya kutoa mchango wao ili kuharakisha zoezi hilo wao wanatatiza kwa njia hii au nyingine, kuwachosha warundi. Haya yanatu kumbusha historia mbaya ya Burundi ;
- Historia ya Burundi
- Kama tulivyojulisha katika matangazo ya chama CNDD-FDD , masuala ya Burundi yamekuwa yakiingiliwa na mataifa ya nje tangu Uhuru wa nchi hadi leo. Mwaka 1961 Mfalme Prince Louis Rwagasore aliuawa kwa sababu ya kupigania uhuru ; uhusika wa baadhi ya nchi za Ulaya ulitajwa na ndiyo sababu hakuna kilichofuatia. Mwaka 1965 waziri mkuu wa kwanza Petro Ngendandumwe alitabiriwa kifo kabla kupitia radio Sauti ya Amerika, mara akauawa na watu wengine wengi, na wengine kukimbia nchi; lakini Jumuiya ya Ulaya ilikaa kimya. Mwaka 1972 na 1973 serikali ya Kapteni Michel Micombero iliua watu kwa mauaji yaliyokithiri ya kimbali. Vilio na kelele za waliokuwa wananyanyaswa havikupewa thamani katika Jumuiya ya Ulaya, huku wakiwepo washauri wa waliokuwa madarakani kutoka nchi hizo. Mwaka 1988 katika tarafa za Ntega na Marangara serikali ya Buyoya nayo iliua watu wapatao elfu tano na kiasi cha watu elfu hamsini kuikimbia nchi kwa misingi ya ukabila asilolipenda ; huku Jumuiya ya Ulaya ikitazama tu bila kumchukulia hatua ikiwa ni pamoja na wenzake. Mwaka 1993 baada ya ushindi katika uchaguzi wa demokrasi, Rais Ndadaye hakujua kuwa yuko na wasaliti waliotumiwa na baadhi ya mataifa ya Ulaya ; ndipo alipouawa katika jaribio la kutaka kumrejesha madarakani Petro Buyoya. Tangu wakati huo wananchi walisimama imara, wakauawa, ikawa vita hasa. Kujitetea kwa wananchi hakukuwafurahisha baadhi ya mataifa ya Ulaya kwani baadhi yao walisema mengi kupiga vita ukombozi wa wananchi kwa sababu ya kuunga mkono vibaraka wao. Je, Jumuiya ya Ulaya ilikuwa wapi mwaka 1996 na1997 wakati zaidi ya warundi elfu tano walipouawa kikatiri na FPR-INKOTANYI wa Rwanda kwenye mto ukivuka kuelekea mjini SHABUNDA katika nchi jirani ya DR. Congo; ni wakati FPR walipotaka kuikamata nchi ya DRC. Wawakilishi wa wakimbizi hao walipiga kelele wakiomba msaada kwa mashirika na mataifa yakiwemo Mataifa ya Jumuiya ya Ulaya, hakuna usaidizi wowote waliopewa hata kulaani maovu huo. Ina maana wakimbizi hao walikuwa wamekwisha hukumiwa kifo. Inasikitisha!
- Ingawa chama CNDD-FDD kilifikia makubaliano na serikali waliokuwa wanapinga baadhi ya mataifa hayo ya Ulaya hawakuridhishwa na maelewano hayo kwani walijua washirika wao wa siku nyingi watapoteza madaraka kamili. Kwa hiyo si ajabu leo kuona yale mataifa tuliotaja ya Jumuiya ya Ulaya yakichukua hatua ya kutaka kuvunja yaliyotokana na mwafaka wa makubaliano hayo na mamlaka za ulinzi na usalama.
- Mwaka 2015, baada ya chama CNDD-FDD kumpitisha Mheshimiwa Rais Petro Nkurunziza ili aipeperushe bendera ya chama katika uchaguzi, baadhi ya Mataifa ya Jumuiya ya Ulaya hawakupendezwa na uteuzi huo, wakaamua kuunga mkono waziwazi walioandaa maandamano haramu na jaribio la kutaka kuipindua serikali. Watu wakauawa, wao wakafumba macho, uzushi na uongo mwingi dhidi ya serikali wakaziba masikio. Mikutano yote iliyofanyika kuhusu agenda za Burundi, wao walitoa shutuma na kuchochea ubaya kwa lengo la kusambaratisha chama na serikali yake. Wakati katika nchi mfano Burkina Faso, Mali na katika mataifa mengine wanapinga sana utumiaji wa nguvu za kurejesha au kuweka serikali za mabavu. Hawakuishia hapo, kwani mataifa hayo yalisitisha misaada iliyoahidiwa nchi ya Burundi kwa faida ya maadui ili kumaliza uongozi wa CNDD-FDD na kushika madaraka. Huu ndio ukweli wa mambo;
- Kwa kuzingatia yote yaliyotajwa hapo juu, chama CNDD-FDD kinatamka yafuatayo:
- Chama kinaomba Jumuiya ya nchi za Ulaya kusitisha hatua zilizochukuliwa kwani matokeo yake yatakuwa ya kuwatenganisha Warundi kama ilivyoelezwa badala yake walete misaada waliosimamisha kwani waliadhibu wasiohusika; na kutoisaidia nchi ya Burundi ni sawa na kuunga mkono wapinzani;
- Chama kinaomba wafadhili kusimamisha misaada na usaidizi wowote kwa waliotaka kuiangusha serikali, kwani bado wanaoendeleza mipango hiyo; badala yake uhisani uwe kwa faida ya maendeleo ya wananchi;
- Chama kinaagiza kukamatwa wale wote waliotaka kuiangusha serikali iliochaguliwa na wananchi; baadhi yao wamejificha katika mataifa ya Ulaya. La sivyo wasimamishwe na kurejeshwa nchini ili sheria ichukue mkono wake;
- Nchi za Jumuiya ya Ulaya zinaombwa kulipa fidia ya hasara kwa serikali kutokana na kusitisha misaada iliyoahidiwa na kutolewa. Hali hiyo ilisababisha kusimama kwa miradi ya pesa hizo;
- Chama kinaomba mataifa ya Ulaya kutofautisha masuala ya kisiasa na ya kisheria (mahakama) ili haki itendeke kwa yahusuyo nchi ya Burundi na kwa mataifa mengine;
- Chama kinakwenda kuanzisha bila kukawia mazungumzo ya wananchi wote yatakayofanyika Burundi na kushirikisha kwa uhuru warundi wote; na kwamba hahitajiki msuluhishi yeyote;
- Chama kinajulisha kuwa mazungumzo hayatakiuka sheria au kuwa mbadala wa sheria/mahakama;
- Chama kinajulisha kuwa hatua zilizochukuliwa na Nchi za Jumuiya ya Ulaya za adhabu kwa baadhi ya warundi wa kabila moja ni kuzubaisha wananchi na mataifa ili kutatiza mchakato wa mazungumzo. Hakuna awezaye kushinda utashi na mapenzi ya wananchi, kwani wakipendacho kinakuwa;
- Chama hakikubaliani na hatua zinazochukuliwa dhidi ya Burundi bila kushirikishwa au kujulishwa ili kiweze kutoa msimamo wake;
- Chama kinawahimiza wananchi kuendeleza mshikamano katika umoja, wajilinde na wanaotaka kuwazubaisha na kuwagawa katika makundi, kwani umoja ni nguvu itakayowafikisha kwenye ushindi kamili;
- Chama kinaendelea kuimarisha amani na utulivu nchini, kwani ni nguzo yamaridhiano ya warundi na nguvu ya kung’oa mizizi ya aina yoyote ya ubuguzi nchini.
- Chama kinaendeleza uhusiano na ushirikiano mwema na udugu na mataifa jirani na mataifa, hata kama kuna uchokozi; kwani chama CNDD-FDD kinajishughulisha zaidi na amani ya Burundi.
Tangazo limetolewa Bujumbura, tarehe 03 Octoba, 2015.
na Mheshimiwa Mbunge Pascal NYABENDA,
Mwenyekiti wa Chama CNDD-FDD.